DijitoStore - Business software

MKUU WA MKOA TABORA AKABIDHI NEMBO YA MKOA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI - TABORA

MKUU WA MKOA TABORA AKABIDHI NEMBO YA MKOA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI-TABORA 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi Dkt Batilda Salha Burina leo Juni 1, 2023, amekabidhi nembo ya Mkoa kwa wanafunzi wa shule ya msingi kutoka shule  mbalimbali mkoani Tabota, watakaoenda kushiriki mashindano ya Michezo ya UMITASHUMTA , ambayo kitaifa yanafanyika hapa mkoani Tabora.
Akikakabidhi nembo ya mkoa, Mhe.Batilda Salha Burian amewataka wanafunzi hao kurudi na ushindi kwenye kila aina ya mchezo kwani serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Michezo wamewekeza kwenye sekta ya michezo ili kuhakikisha Tabora inasonga mbele kimichezo.

Ametoa pongezi kwa Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa fedha ili michezo hii kufanyika mkoani Tabora, na kutoa nafasi kwa wanafunzi kukuza vipaji vyao.
kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post