TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

TWENDE KWA MPARANGE 01

TWENDE KWA MPARANGE
MTUNZI: AMANI H. KIGOYE
SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
"Hapa ndio buza bwana sehemu maarufu kwasasa katika jiji la Dar." Alisikika dalali mmoja aliyekuwa anazungumza na kijana aliyekua anatafuta chumba.

"Sijajua kwanini hili eneo limekua maarufu hivi karibuni na hali ya kuwa huko nyuma hakukuwa maarufu hivi!?" Kijana aliuliza swali huku wakiwa wanednelea kutembea.

"Umesema unaitwa nani!?" Akisimama na kumtazama usoni.

"Naitwa Suma."

"Aahhaaa ok! Sasa sikia Suma nikueleze kitu…," akitengeneza suruali yake iliyokuwa inamshuka.

Kujana anayeitwa Suma alitulia na kumtazama dalali wake huku akiwa anaonekana anasubilia kwa hamu hiko kitu ama jambo analotaka kuelezwa.

"Huku sio kama hakukuwa maarufu, tangu zamani huku kulikuwa maarufu sana, kipindi hiko sisi tunakaa kigilagila pale tulikuwa tunakuja huku kutungua maembe na ilikuwa ikisifika kwa matunda hayo."

Suma alijikuta akishangaa huku akianza kupiga hatua maana aliona kama jamaa akamjibu tofauti na swali alilomuuliza.

"Sio huko Suma ni huku." Akiwa anakatisha kwenye kichochoro kimoja kilichokuwa chembamba sana.

Haraka Suma aligeuza na kuanza kumfuata mwenyeji wake maana yeye huko hakua mwenyeji kabisa.

"Umesema unafanya kazi gani!?"

"Ni injinia."

"Ok! Kumbe injinia, kituo chako cha kazi?"

"Niko hapo airport kipawa na ndio maana nimeamua kutafuta karibu na sehemu yangu ya kazi."

"Kweli kabisa maana hapa na hapo kipawa hata sio mbali ni gari moja tu umefika."

Waliendelea kuzungumza huku wakiendelea kupita kwenye kile kichochoro ambacho hakikuruhusu wetu wawili kupishana, hivyo iliwabidi wstu wengine wa upande wa pili wasimame pembeni mwanzoni mwa uchochoro mpaka wakina Suma watakapomalizia kupitia ndipo na wao wapite. Huko ndio iswazi bwana ama unaweza ukasema Uswahili kweli kweli na yalikuwa majira ya mchana hivi na hata hao wakina mama na baadhi ya vijana waliokuwa wanawasubilia wapite walikuwa wameshika vibunds vya karatasi mikononi mwao vikiwa vimenona mafuta. Walikuwa wametoka kununua samaki wa kukaanga, ashua na miguu ya kuku ama vichwa kwa ajili ya kwenda kula ugali wa mchana. Unazani huko watu wanashida na masuala ya mboga? Wewe songea ugali mboga zipo zimejazana ushindwe wewe tu na pesa yako, halafu hata sio gharama kivile mpaka hamsini huko Uswahili inatumika Yani utapata ngozi za kuku kwa hamsini yako na yupilipili twa maana uende ukaule ugali wako.

"Za sahizi jamani!?" Alisikika yule dalali akiwasalimia waliokuwa wanasubiri wapite.

"Salama." Mama mmoja akaitikia.

Suma akabaki kushangaa wale wenyeji wake waliokuwa wanamtazama yeye kwa jinsi alivyokuwa smart na wakijua kabisa ni mgeni mitaa ya huko.

"Shikamooni!?" Suma alisamia lakini wakina mama kama wawili wstu wazima walibaki kumtazama kwa kumshangaa.

Suma alijikuta akijisikia vibaya baada ya wale wakina mama kutoitikia salamu yake. Waliendelea kumtazama akiwa anawapita huku wakionekana kabisa wenye mshangao mkubwa hadi alipopita na nyuma yake wakaangua kicheko kizito cha umbea.

"Hebu twendeni basi jamani." Alisikika mvulana mmoja aliyekuwa amevaa kipenzi kifupi cha jinzi huku akiwa anataka kutangulia mbele.

"Wewe Dully hebu jiheshimu huko utapitaje kabla yetu." Mwanamama mmoja alihoji huku akimuwekea mwili kumzuia.

"Sasa mmekaa kucheka tu."

"Hebu rudi nyuma huko, ndio kusema unaharaka sana ama?" Mama mwingine aliyekuwa amejichubua uso wake nayeye alidakia akiwa anamrudisha Dully nyuma kwa kumvuta.

"Sasa wewe mama Salimu neng'eneka unimwagie vidagaa uduvi vyangu utanibeba." 

"Kwani kukubeba shilingi ngapi?"

"Hebu twendeni basi jamani tunacehelewa wengine." Alisikika msichana mmoja aliyekuwa amevaa sale za shule huku mdomo ukiwa umempauka kwa njaa na ndio alikuwa anatoka shule kwa siku hiyo ya Ijumaa.

Waliendelea kubishana huku wakiwa wanapita kwenye kile kichochoro na mbele yao watu wengine wakiwa wanawasubilia na wao. 

"Hii ndio mitaa yetu bwana kwa hiyo uvumilie njia zetu." Dalali aliongea akiwa anaruka dimbwi la maji machafu na kwenda kukanyaga jiwe la pembeni.

"Angalia Suma usikanyage."

"Kwani tunakwenda mbali sana!?"

"Hapana tushafika ni nyumba ile pale mbele." Akiwa anamuonesha kwa kidole.

Ulikuwa ni mtaa fulani uliochangamka sana huku ukionekana kuchakaa kwa rangi nyeusi na yote hiyo ni kwasababu baadhi ya madimbwi kujazwa vifusi vya chenga za mkaa. Na isitoshe mtaa mmoja kulikuwa kuna wauza mkaa kama watatu na wote wakiwa wanastoo za maana, kwa mbele kidogo kulikuwa kuna kigenge mshenzi ambacho kilikuwa kina kila kitu kwa ajili ya mahitaji ya jikoni na kulikuwa kumechangamka kweli kweli. Kelele za miziki zilianza kumpokea kijana Suma na alipotupia macho pembeni aliona kuna spika kubwa zimepangwa nje ya maktaba moja ya kukodisha Cd za filamu na kubani miziki. Akitazama Suma kwenye kile kibanda ama ile maktaba kisha akagonganisha macho yake na kisichana kilichokuwa kimejaa dela moja jekundu huku amelishikilia kiasi cha kufanya paja lake la mguu mmoja lionekan sawia. Haraka akakwepesha macho na mbele kidogo akakutana na watoto wakicheza mpira barabarani kwa kupigiana huku wakiwa wanatoka shule.

Waliendelea na safari yao kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa ameelekezwa na hata kabla hawajawapita wale watoto waliokuwa wanacheza mpira ghafla ulionekana mpira kupita usoni mwa Suma na kwenda kutua kwenye sahani ya sambusa iliyokuwa upande wa pili na kumwagika chini. Watoto wale baada ya kuona hivyo haraka wakakimbia na kila mmoja akaingia kichochoro chake huku wakisikia baadhi ya watoto wakiita kina la mama mwenye hiyo biashara.

"Mama Saidi…!?" Alisikika msichana mmoja wa makamo akiita huku akiwa anakimbilia ndani.

Muda wote huo Suma alikuwa anatazama na kusimama kuona nini kitatokea, na kumfanya dalali abaki akishangaa na kutabasamu.

"Suma twende bwana ndio mambo ya uswahili hayo, mbona kawaida."

"Kawaida!?"

"Ndio!"

"Kawaida mtu biashara yake umeagwa?"

Wakati wanaendelea kuongea huku wakiwa wanaondoka taratibu mara alionekana yule mwanadada aliyeingia ndani kwenda kumuita mama Saidi akawa anatoka akiongozana na mwanamama mmoja mnene kiasi akiwa amevaa dela limepauka na lina unga unga kila kona na limechanika kwa chini hadi usawa pajani. Huko ndani alikuwa amevaa taiti moja nyeusi iliyokuwa imembana mwili wake hadi chini kiasi cha kuacha vikuku alivyokuwa amevaa kwenye kila mguu vuonekane vyema. 

"Nani aliyefanya huu upuuzi!?" Mama Saidi aliuliza kwa hamaki.

"Watoto wa mama Dondo na yule mjukuu wa mzee Tumbae." Yule binti alijibu huku akiwa amebinua midomo na vidole vikiwa juu.

"Leo watanijua mimi nani." Huku mwanamke akitoa mtandio wake aliokuwa ameufunga kichwani na kuufunga kiunoni kama anafunga mzigo wa kuni.

Suma akabaki akishangaa na huku mama Saidi mwenyewe akimpita kama gari bovu na kumuachia harufu fulani ya jasho na kumfanya abaki akishangaa na kukunja uso. Huko nyuma ya mama Saidi walionekana sasa wapambe na wao wakimfuata huku wakiongea na kumpambiza mama wa watu. Wanakwambia vita vya panzi furaha kwa kunguru wakiwa wachache wamebeba sinia la sambusa na sambusa zenye michanga huko nyuma yao walionekana watoto wengine baadhi wakiokota sambusa zilizokuwa na hali mbaya kisha wakawa wanakula.

Huku ndio Uswahili wewe kitu kikianguka tunakipangusa michanga kisha kinakwenda kinywani, unashangaa kwa hao watoto kuokota hizo sambusa? Mbele tu karibu na nyumba ambayo anatakiwa kwenda kuoneshwa Suma akakutana na mzee mtu mzima akiwa anapita samaki wake chini aliyeanguka baada ya kumnunua na kumpangusa michanga na kumfunga tena kwenye karatasi. Hayo yote Suma akawa anashangaa maana hakuzoea kabisa na hiyo yote ni kutokana na kuishi maisha safi ya hali ya juu akiwa nyumbani kwao na sasa ndio kwanza alikuwa anataka kuanza maisha ya kujitegemea. 

"Duh!' alibaki akijigunia huku dalali akiwa anagonga geti lilipo mbele yao.

"Tena hii nyumba kidogo inautulivu na inageti kwa hiyo mnakuwa ndani kwa ndani." Dalali aliongea akiwa anajichekesha na kumtazama Suma wakati wanasubilia geti lifunguliwe.

Suma sasa ikambidi ageuke kutazama hiyo nyumba yenyewe, kwanza hilo geti lilikuwa limechoka na limeliwa na kutu kiasi cha kujiuliza lilikuwa lina rangi gani. Maana lilikuwa limebanduka banduka rangi na kufanya rangi ziwe nyingi zimebebana. Suma akiwa analishangaa geti hilo jinsi lilivyo chakaa na hata wezi wakisema waje kuingia basi walikuwa wanaingia kiurahisi sana, mara likafunguliwa na akonekana mama wa makamo akichungulia na alikuwa mwenye asili ya kipemba.

"Karibuni!" Huku akifungua mlango.

"Asante!" Wote wawili waliitikia kisha dalali akaanza kuzungumza.

"Mama Jamila…! Yule kijana niliyekwambia ndio huyu hapa nazani nimekuja naye ili apate kukiona hiko chumba."

"Aahhaaa! Basi sawa karibuni ndani." Akiwapisha wapite.

Suma na dalali wake waliingia ndani lakini ile wanaingia ndani wakapokelewa na sufuria moja lililorushwa na kwenda kutua ukutani tokea upande wa pili. Wakiwa wanalishangaa lile sufuria mara wakaanza kusikia sauti za watu wakitukanana na purukushani za maana. Kwanza Suma akamtazama dalali na dalali akamtazama mwenye nyumba na yeye mwenye nyumba akabaki kutabasamu.

"Msijali kuna wasichana kidogo wamepishana kauli." Huku akiwa anaingia kwenye nyumba kubwa na kuwaacha wakina Suma wakimsubilia.

Huko nako kwenye vyumba vya uwani upande wa pili ambako walikuwa hawapaoni kelele za kutukanana zikiendelea na sauti za mtoto mdogo akilia. Vishindo vikaongezeka na hatimaye sasa wakashangaa kuona wasichana wawili wakipigana na kukamatana miilini mwao. Ilikuwa ni aibu na ajabu maana walikuwa wanapigana huku wamevuana nguo, mmoja alikuwa amebaki na chupi tu huku chuchu zake zilizomsimama zikiwa zinacheza cheza huku mwingine akiwa amebaki na sketi fupi na shanga baadhi zikiwa zinaning'inia na nyingine zikiwa zimekatika na kusambaa chini. Wakati wanaendelea kupigana na kuja usawa waliokuwa wamesimama wakina Suma nyuma ya yule mwanamke aliyekatiwa shanga zake kulikuwa kuna mtoto anayelia na kumvuta huyo mwanamke maana ndiye aliyekuwa mama yake.

"Malaya mkubwa wewe umekosa wanaume huko nje kote ndio umeona mme wangu wa kutembea naye mbwa wewe." Huku akimshushia kofi la uso yule msichana.

Ilikuwa pige nikupige hapo na hata sekunde hazikupita huko kwenye geti walisikika watu wakichungulia na kushangilia. 

"Haya na nyie mnataka nini hapo!?" Alisikika mama mwenye nyumba akifoka na kumkabidhi funguo dalali na kwenda kwenye karo kuchukua beseni la maji machafu.

"Anakuja anakuja..!" Walisikika watu waliokuwa wamesimama nje ya geti wakichungulia ule mtanange wakisemezana huku vishindo vya kukimbia vikisikika.

Mama mwenye nyumba alilinyanyua lile beseni la maji machafu na kuyamwagia getini na waliokuwa huko habari waliipata kisha mwanamke akaenda kulifunga na geti lenyewe. Huku ndani watu waliendelea kuzinyuka na mama mwenye nyumba hakuonekana kujali ndio kwanza akawa anakwenda kuwafungulia chumba pembeni na eneo walilokuwa wamelazana wale wanawake.

"Jamani chumba ndio hiki hapa…, hebu na nyie sogeeni huko " akiwa anawasukuma wale waliokuwa wanapigana.

Suma alikuwa anajionea ajabu maana wale wanawake walikuwa wameumizana usoni kwa kukwanguana na kucha zao hadi zamu zikawa zinawataka halafu wenyeji wake wakawa wanaonekana hata hawajali. Waliingia kwenye chumba kuendelea kukikagua huko nje bado varangati lilikuwa likiendelea, sasa ikawa hakuna kutukanana bali ikawa ni miguno na makofi tu ndivyo vilivyokuwa vikisikika na ile sauti ya mtoto kulia. Ukaguzi uliendelea mwishoe huko nje ukasikia ukimya na hata mtoto nayeye akawa yuko kimya na ndipo walipomaliza kukagua na Suma alionekana kuridhika nacho.

"Kwa hiyo utalipa kabisa nikuandalie mkataba ama?"

"Ndio nitalipa kabisa na nazani mpaka kesho kutwa nitakua nimesha hamia." Suma alijibu akiwa anatoa pesa mfukoni na kuanza kuhesabu.

ITAENDELEA

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post