TWENDE KWA MPARANGE
MTUNZI: AMANI H. KIGOYE
SIMU: +255766416862
SIMULIZI MIX ENTERTAINMENT
SEHEMU YA 02
Suma alikuwa anajionea ajabu maana wale wanawake walikuwa wameumizana usoni kwa kukwanguana na kucha zao hadi zamu zikawa zinawataka halafu wenyeji wake wakawa wanaonekana hata hawajali. Waliingia kwenye chumba kuendelea kukikagua huko nje bado varangati lilikuwa likiendelea, sasa ikawa hakuna kutukanana bali ikawa ni miguno na makofi tu ndivyo vilivyokuwa vikisikika na ile sauti ya mtoto kulia. Ukaguzi uliendelea mwishoe huko nje ukasikia ukimya na hata mtoto nayeye akawa yuko kimya na ndipo walipomaliza kukagua na Suma alionekana kuridhika nacho.
"Kwa hiyo utalipa kabisa nikuandalie mkataba ama?"
"Ndio nitalipa kabisa na nazani mpaka kesho kutwa nitakua nimesha hamia." Suma alijibu akiwa anatoa pesa mfukoni na kuanza kuhesabu.
"Ulisema kiasi gani!?" Suma aliuliza.
"Ni elfu 40 tu kwa mwezi huku vyumba sita bei kama huko mjini."
"Ok sawa nitalipa ya miezi sita." Akiwa anaendelea kuhesabu.
Baada ya kumaliza kuhesabu alichomoa noti kisha akamkabidhi mwenye nyumba na yeye akawa anazihakikisha, baada ya kuhakikisha alimtazama Dalali kisha akamtazama Suma na kufungua mlango.
"Haya twende tukaandikishiane." Huku akitoka nje.
Walitoka na kukuta wale waliokuwa wanapigana kila mmoja amekaa mlangoni kwake akiwa hoi na mwingine akiwa anabembeleza mtoto wake. Mama mwenye nyumba aliwatazama kisha akatabasamu na kwenda zake ndani akiongozana na kina Suma. Masuala ya kuandikishiana yalianza na baada ya muda mfupi walimaliza kisha Suma akakabidhiwa chumba na kuondoka zake na mkataba wake.
KARIBU BUZA KWA MPARANGE.
*********
BAADA YA SIKU TATU
Alionekana Suma na wenzake wakiwa wanatoka kazini na kwenda kwenye kituo cha mabasi kwa ajili ya kuelekea majumbani mwao.
"Mzee hivyo vyumba bei yake haishikiki mazee." Alisikika kijana mmoja aliyeitwa Aidan.
"Mh! Mimi kwanza mpaka nimechoka na kuamua kutulia kwa aunt mpaka nitakapopata mshahara wangu wa kwanza."
"Mnalia lia vijana." Suma alidakia maongezi ya wenzake huku wakiwa wanajiandaa kuvuka barabara kwenda upande wa pili wa kituo kinachofahamika kama uwanja wa ndege.
"Wewe naona huwazi wala huumii suala la bei ya vyumba." Aidan alimuuliza Suma.
"Hata mimi namuomba." Daniel naye akadakia.
"Itakuwa ameridhika kukaa nyumbani kwao."
"Yani nitoke mbezi ya kimara kila siku kuja kazini mzee na navyowahi hivi?" Suma aliwauliza.
"Sasa kumbe unataka kusema unaishi wapi kwa sasa?"
"Mimi naishi nyuma tu hapo ya airport."
"Wapi!?" Wote wawili walijikuta wakiuliza kwa pamoja.
"Kiwalani hapo!?" Aidan aliuliza.
"Hapana."
"Sasa wapi bob? Si useme basi."
"Naishi buza hapo, vyumba bei poa halafu vikubwa mazee."
"Mh!" Wote wawili walijikuta wakiguna na kumtazama mwenzao.
"Sasa nini mbona mnashangaa?"
"Yani ukakae buzz kweli wewe kwa jinsi navyokijua mzee wa Bata?" Daniel alidakia.
"Kuna muda ukifika lazima ukubali umekuwa na uache masuala ya kula Bata na uanze kujenga maisha yako."
"Unamaana gani?"
"Nimeamua kwenda kuishi buza kwasababu nahitaji kuanza maisha na kuanza kujifunza maisha bila usimamizi wa wazazi."
"Kiasi gani kodo huko!?" Aidan aliuliza.
"Nalipa elfu 40 tu kwa mwezi."
"Mh! Oya muda mwingine uwe siriasi basi bob."
"Kama hutaki basi."
"Kiwalani kwa kude, kigilagila buza tandika hiyo…!" Alisikika mpiga debe mmoja mwenye sauti ya kukoroma akiita huku akiwa anakimbilia gari la tandika.
"Oya mazee gari hilo halafu jeupe kibosi." Suma aliongea akiwa anakwenda kupanda gari.
"Hivi huyu fala yuko siriasi kumbe!?" Aidan alimuuliza Daniel.
"Mh! Itakuwa kweli."
Gari aliyopanda Suma iliondoka na kuwapungia mkono huku akiwa anatabasamu usoni mwake na kuwafanya sasa wenzake wabaki na mshangao.
"Oya kwani kuna shida gani nasisi tukienda buza!?" Daniel alimuuliza mwenzake.
ITAENDELEA
Tags
Simulizi 🔞