Story.... *LIVIA*
SEHEMU YA 1
Naitwa livia Samson nyirenda,nilizaliwa mbinga songea kwa wazazi wangu ambao nao waliaga dunia wote kwa ugonjwa usioeleweka nikiwa darasa la sita.mm ni mtoto wa pili kwetu wakwanz akiwa kakangu samwel.kaka sam na mm tulipishana miaka mingi kidogo nay eye alibahatika kusoma akawa mwalim wa shule ya msingi,wakati mm niliishia darasa la saba na kuendelea kukaa kwenye mji wa babangu na mamangu huku nikiwa napewa chakula na ndugu ikiwemo kaka.maisha yalikua magumu sababu hata wazazi wetu hawakuacha kitu nyumbn zaidi ya nyumba tatu ambayo moja kubwa ya bati,kuna ingine jiko na ingine stoo ya mazao mana walikua wanalima sana na hizo zilikua za nyasi.kutokana na ugumu wa maisha ilinilazimu na mm kufanya kazi mbali mbali za vibarua kama kulima,kumwagilia bustani na kazi yoyote iliokua inanijia mbele yangu,pamoja na yote nilikua sikosi kanisani kwa kazi mbalimbali za kanisa nafanya hata kusidia masista kazi za hapa na pale wananipa pesa na zawadi mbali mbali kama nguo sabuni hata chakula na hayo ndio yalikua maisha yangu.mabinti wengi walikua wamechangamka sana wamejiunga na makundi ikiwemo kuwa na wanaume lkn mm sikuwa hivo.japokua nilikua nashawishiwa na wanaume mbali mbali kufanya hivo sikuwahi kubali hata siku moja nilikua nimekazana kujitaftia maisha huku nikiamini kabisa kuna siku Mungu atanipa mtu sahihi kabisa wa kuishi nae.sikuwahi kutamani kuwa tajiri mana kuna watu wenye uwezo nilikua nawafanyia kazi nilikua nawaona vile maisha yao hayana raha hasa wanawake wananyanyasika na wanaume zao sababu tu wanapesa wanaume wanakua sio waaminifu hivo sikuwahi kabisa waza kuwa na maisha ya dizaidi hio.nilipendwa sana na watu wengi sababu ya tabia yangu hivo na mm nilijitahidi sana kuwa mtoto bora.siku moja nilikua nafanya kazi ya kufua kwa mama mmoja hivi n mke wa tajiri,mara akaja mtoto mmoja wa mtaani kwetu akaniambia naitwa na sister magret kanisani,nikasema sawa nitaenda,akasema uwahi mana amesema ni muhimu sana uende,nikasema sawa namalizia kufua kisha nitaenda.nilifua haraka nikapewa pesa yangu japo ndogo kulingana na nguo zenyewe lkn ni bora kuliko kutokua na pesa kabisa.nilitoka pale moja kwa moja nikaenda kanisani kwa sister mage.nilifika nikakuta gari moja zuri pale nje,nikajua watakua mapadre wamekuja labda,nilienda moja kwa moja kwenye nyumba ya masista nikagonga akafungua sister mage,alivoniona akafurahi akasema karibu sana mwanangu liv,nikasema asante shikamoo,akasema marahaba,ingia ndani,nikaingia,nymba yao ilikua nzuri ina kila kitu ndani kama nyumba za watu matajir,seblen nilikuta amekaa mama mmoja mnene mweupe hivi yupo na watoto wawili wadogo kama wana umri wa miaka minne hiv ni kama mapacha mana wanafanana sana,nikamsalimia Yule mama akaitikia kwa furaha sana,nikakaa,sister mage akasema nenda kapakue chakula kwanza ule ,nikasema asante ssita nimeshiba,akasema mmmh liv ebu nenda bana kwani huko umekula pilau ya kukua wewe?nikainama kwa aibu nikasema hapana ngoja nikapakue basi,akacheka akasemahaya nenda,nilinyanyuka na kwenda jikoni nilipakua msosi akasema uchukue na juice kwenye frij,nikasema asante sana,nikapakua nikawa nakula kule jikon,akasema wee mbona huji jmn?nikasema nakula huku,akasema njoo huku tuna maongezi na wewe,nikasema sawa nilibeba chakula changu nikaenda seblen,nikakaa kwenyey sofa mara mtoto mmoja akajimwagia juice na ikamwagika chini,niliweka chakula chini na kumkimbilia nikamnyanyua asiendelee kuloa kisha nikaedna nae jikon nikamfuta nikachukua dekio na ndoo ya kudekia nikaweka maji na kwenda seblen nikadeki pale,Yule mama alikua ananiangalia sana huku anatabasam,nilimaliza nikasuuza dekio nikasuuza na ndoo nikaweka mahali pake,nikarudi kukaa,sister akasema liv huyu ni dadangu anaishi dare s salaam,ni dadangu kabisa tumbo moja,nikasema nafurahi kumfahamu,akasema sasa huyu dadangu anashida sana ya msaidizi wa kazi za ndani na mm naona kabisa wewe unaweza mfaa mana dadangu ana upendo na mpole sana,na wewe pia utapata nafasi ya kupata pesa nzuri ili uweze kujitegemea kuliko kuhangaika na vibarua vigumu kila siku,atakulipa sh elf 60 kila mwezi mana yy ana watoto watatu mmoja yupo darasa la tano na wengine ni hawa hapa,dadake akasema hapana nitamlipa 70 ila awe tu anafanya majukumu yake,mmh niliwaza 70 elfu sabini?sijawahi ishika maishani gafra naenda kuosha vyombo kulea watoto tu nilipwe hio?siwezi kataa,lkn pia siwezi kubali tu mapema,nikasema sawa nimeskia lkn naomba kwanza niongee na kina babamdogo na kina mamdogo na kaka pia,akasema sawa haina shida,nilimaliza kula nikaosha vyombo vyote mana hata walivyolia wao vilikua jikoni kisha nikamaliza,nikafuta na kuvipanga.sister akasema mama crey (dadake)anatarajia kuondoka kesho kutwa jitahidi basi muende wote sawa?nikasema sawa.nilienda moja kwa moja kwa babamdogo ambae alikua ananilea sana nikamweleza akasema una uhakika na unakoenda?nikasema ndio ni dadake sister kabisa,babamdogo akasema nataka nimuone aje yeye akuombe hapa asije kukuchukua ukanyanyasika huko,nikasema sawa.nilitafuta simu nikampigia kaka ambae alikua anafanya kazi morogoro nikamweleza akasema dar sio mbali na morogoro nenda ukajitaftie maisha,nikasema sawa.nilienda kwa sister nikamwambia alivosema baba mdogo nao akasema haina shida panda kwenye gari twende,nikapanda kwenye ile gari nzuri tukaenda kwa bamdogo wakaongea nae akakubali wakamuachia na pesa kisha tukaenda kwa mamdogo nae akakubali na kutoa Baraka zote,wakasema basi mtoto wa bamkubwa alieachika karudi na watoto ndio akae pale nyumbn kulinda mji,nikasema sawa.walirudi kwao mm nikafua nguo usiku huo japo nilikua na nguo sio nyingi na zimechoka lkn safi mana nilipenda sana kuwa msafi siku iliofata zilikauka nikaweka kwenye shangazi kaja yangu jioni nikaaga ndugu kisha nikaenda kwa sister,nilisaidia kazi mbali mbali tukala jioni tukalala alfajir safari ya dar ilianza.mama crey mwenyewe alikua anaendesha safari ilikua nzuri nilikua naoneshwa maeneo na miji mbali mbali,sehemu nzuri tulikua tunasimama tunaangalia tunakula safari inaendelea,tulifika morogoro usiku mida ya saa mbili,mama crey alichukua hotel tukalala mm na watoto yeye peke ake kesho yake saa mbili tukanywa chai safari ya dar ikaanza,nilifurahia sana safari mana niliijua miji vizuri nilimpenda sana mama crey alionesha upendo sana kwangu.tulifika mida ya saa tano kwake,alikua anaishi kawe nyumba kubwa sana ina geti zuri,nje kulikua na magari manne yamepak ni wazi alikua tajir.alinikaribisha akasema livia karibu hapa ndio nyumbn,nikasema asante sana,tulishusha mizigo aliokua amenunua njiani tukaingiza ndani,nilishangaa uzuri w aile nyumba,jmn watu wanaishi nyie sisi tunasindikia tu maisha,alinipeleka chumbn kwangu akasema hiki ndio chumba chako,kilikua kizuri tu kina kitanda kikubwa nacho ni kikubwa,akasema najua umechoka na safari livia lkn hapa ndnai n mm na wewe tu wakubwa na mlinzi yuko nje,leo hatutopika mchana tutaagiza nje ila usiku mwaya tutapambana,nikasema sawa,akasema bafu lipo hapo ndani na choo oga pumzika na mm naenda pumzika,nikasema sawa mama,niliigia bafuni nikaoga,sikuwa mgeni sababu hata kwa masista wana mabomba kama hayo,nilipomalizanilipanda kitandani nikalala,niliamka baada ya masaa kadhaa nikatoka nikakuta mama bado amelala,niliwaza nifanye nn nikaona kama nyumba ina vumbi,niliangaza huku na huko nje nikazunguka nyumba nzima nje nikaona kuna madekio na ndoo nikachukua nikaja ndani nikaenda jikon nilikua nakisia tu nikaona vitaulo,nilichukua nikafuta futa seblen nikafuta jikoni,yani nilifanya usafi kila kona.kulikua na vyombo vichafu pia sikujua nani ametumia nilivomaliza usafi nikaanza kuosha vilevyombo huku nikiimba imba,mara mtu akanitekenya kwa nyuma nilistuka nikageuka alikua ni mbaba mbaba hivi mwembamba lkn alikua anajichekesha…..
Tags
simulizi