Riwaya:SIRI YA MOYO.
Watsapp:0747995035.
SEHEMU YA NNE (04)..
Kitendo ambacho kilizidi kumshangaza zaidi Misholi,binafsi alijua nini binti huyo anataka kutoka kwake ila ilimbidi akaushe tu asije akaharibi cv yake akaonekana yeye ni mhuni ili hali kila mmoja pale shuleni na hata mtaani anamtambua kama mtumishi wa Mungu."Misholi naomba basi uwe unanisaidia somo la hesabu kunifundisha maana mimi kwa kweli ni mbovu mno kwenye somo hilo".Aliongea Diana huku akifungua fungua kurasa za makaratasi ya Misholi."Kwa hilo tu,ondoa shaka kabisa wala usijali kabisa,mimi nipo kwa ajili yako".Alisema Misholi na kumfanya Diana aanze kuachia matabasamu ya waziwazi bila kuficha."Haya,nilikuwa na hilo tu,ngoja nikuache uendelee kujisomea nisije nikakuharibia mudi".Baada ya Diana kumaliza kuyazungumza maneno hayo, alisimama kisha akaondoka pale akirejea sehemu yake na kukaa,,,Muda wa mapumziko ukamalizika hatimaye wanafunzi wote wakarudi madarasani kuendelea na masomo.Neema pamoja na Cathe nao wakaingia kwenye darasa lao na kwenda moja kwa moja hadi maeneo yale aliyokuwa akikaa Diana kwani hata wao siti zao zilikuwa pale pale,,,baada ya kukaa tu kabla walimu hawajaanza kuingia madarasani,Neema alimshtua Diana,Diana alipogeuka Neema alitabasamu huku akiyaangaza macho yake huku na huko."Mh!! Best naona siku hizi umeanza kuchangamkia fursa si mchezo". Aliongea Neema,Diana akamkazia macho ."We acha,akhaa mimi wala sichangamkii fursa".Alitamka Diana,na kabla mazungumzo yao hayajaendelea mwalimu wa somo la Kiswahili aliingia na huo ndo ukawa ukomo wa story yao kwa muda huo.Basi masomo yaliendelea mpaka mishale ya saa nane,mida hiyo ikawa ni ya wanafunzi kurudi makwao.Misholi kwa upande wake alichomoka kimya kimya peke yake bila ya kuambatana na mtu hadi kwao,Diana alipomtafuta ili waongozane hakumuona,akahuzunika sana.
"Eti Neema!! Umemuona Misholi?" Diana alimuuliza rafiki yake huyo huku akiendelea kuyazungusha macho yake ili kujaribu kumtafuta kijana huyo kama atafanikiwa kumuona."Hapana,sijamuona,huenda amekimbia nyumbani,si unamfahamu Misholi jinsi alivyo?" Neema alijibu kisha akauliza swali muda huo huo."Basii sawa".Alisema Diana huku akilamba lips zake."Vipi mbona sikuelewi Diana,kwani una inshu gani na Misholi maana naona upo na kasi ya four g".Aliuliza Neema."Ni siri yangu jamani,ila siku nikihitimu chuo kikuu kila mmoja atajua ni inshu gani nipo nayo kuhusiana na Misholi". Alizungumza Diana mara hii wakianza kutembea kuikamata njia ya kurudi makwao,,,Sasa wakati wakiwa wanaendelea kutembea namna hiyo tena kwa mwendo wa taratibu,wajuba kadha wa kadha waliokuwa wanawaona walibaki wakisemezana wao kwa wao huku wakiwamezea mate wasichana hawa warembo.
"Jamani tutafuteni tu elimu,bila hivyo wasichana kama hawa hatuwezi kuwapata".Kijana mmoja mfupi na aliyekuwa amejazia kifuani aliongea baada ya kumalizia kumtazama Diana."Elimu kitu gani wewe? Ungesema tutafute pesa ningekuelewa na si kusema eti tutafute elimu".Jamaa mweupe furani hivi alipinga."Hapana broo,pesa utazipata baada ya kusoma na kufika huko...kufika huko chuoni na ndio maana nikatamka hivyo".Kijana yule mfupi akazungumza tena.Wakati wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao hayo,katikati yao akaingia kijana mmoja aliyekuwa akiitwa Simoni,yeye akaanzisha mada nyingine tofauti kabisa."Jamani,Yesu anawapenda achaneni na mawazo mfu mfu ya kuiwaza sana dunia,maana dunia itapita na mambo yake yote na hukumu ya Mungu yaja,tubuni muache dhambi".Simoni aliyazungumza maneno yale,vijana wakamcheka sana na kisha kuanza kumdhihaki vibaya."We jamaa utakuwa umerogwa wewe,hata kama ni ulokole,huo siyo ,huo ni ulimbukeni.Hizo ni story za sungura na fisi tu,,,wazee wetu tangu wanazaliwa mpaka wanazeeka huyo Yesu haji tu,sasa wewe chalii unae nuka maziwa unasemaje,na utatuambia nini ili tukuelewe?".Yule kijana mfupi alizungumza."Hahaha!! Mzee mwambie huyo,Halafu anatuambia eti tuachane na dhambi,yeye mwenyewe hapo alipo huenda anafanya dhambi nyingi tu kwa siri,kwa hiyo asitupayukie hapa".Mwenzake akamsapoti.
"Meseji send and derived,,,mimi ujumbe nimeufikisha na sina muda wa kujibizana na nyie". Aliongea Simoni kisha akaachana nao na kuelekea moja kwa moja hadi pale kwa kina Diana,akaungana nao katika mwendo wa kutembea.Sasa pamoja na utumishi aliokuwa nao kijana Simoni hakuwa na rafiki ,na hakuna aliyekuwa akimpenda,si wasichana na si wavulana na hata huko kanisani katika kanisa lile waliko kuwa wanasali hakuna aliyekuwa akimpenda zaidi ya mchungaji tu,,,mama mchungaji hakuwa akimpenda kijana huyu ,kiufupi hakuwa akimkubali kabisa,kwa madai ya kwamba yeye ni mhuni na hafai jambo ambalo lilikuwa si la kweli,maana Simoni hakuwa mhuni kama alivyokuwa akifikiria sema tu kijana huyo hakuwa na nyota ya kupendwa.Simoni alikuwa akisali kanisa moja na kina Diana na pia walikuwa wakisoma darasa moja,,,Sasa huko kanisani hata apewe vipi nafasi ya kuhubiri na mchungaji hakuna aliyekuwa akimkubali wala kuyakubali mahubiri yake.Tofauti na Misholi,huyu akisimama kuhubiri watu wanashangilia vibaya sana huku wakimsifia kuwa anajua kuhubiri na ni mtumishi mzuri.Hata hivyo kijana Simoni hakuwa na shida nao aliamini ipo siku watamheshimu tu hata kama itakuwa ni baada ya miaka arobaini.Sasa akiwa anatembea na kina Diana namna ile, wasichana hawa walijisikia vibaya mno kuambatana na jamaa kama huyu,kila wakimtazama na sura yake ilivyo wanaona kama wapo na sokwe tu pale ."Hebu tutembee haraka haraka bwana,huyu jamaa akianza kuongea tu ni sawa na kimefunguliwa choo maana huwa ananuka mdomo".Cathe aliwanong'oneza wenzake wakamtazama chini chini Simoni na muda huo huo wakaanza kuongeza mwendo wa kutembea.Muda mfupi baadae Simoni akaachwa nyuma ,na alipojaribu tu kukazana na yeye ili wasimuache hapo ndipo walipoamua kumfungukia waziwazi Simoni ukweli wa mambo.
***********************
"Tutokee bwana hivi huoni hata aibu,unanuka mdomo na majasho bwana,tutokee". Aliongea Cathe,Simoni hakumjibu chochote zaidi ya kumkazia macho tu."Usitutolee mimacho yako we sokwe mtu ondoka tu maana unatutia nuksi tu hapa".Neema aliongea,neno lake hilo likamshangaza sana Simoni maana hakutegemea kama Neema huyu huyu anae imba mpaka kwaya kanisani anazungumza maneno ya chuki kama hayo."Neema dada yangu,tafadhari usikufuru namna hiyo dada yangu,kumbuka mimi nami ni binadamu kama nyie hata kama nina sura inayofanana na sokwe!! Halafu dada angu,hii dunia ni kubwa sana japo hakuna uhakika wa kuikaa milele.Pia kumbuka wewe umeokoka,hutakiwi kuwa na chuki kama watu wa mataifa, tafadhari dada angu ni vyema ukabadirika". Aliongea Simoni,sasa wakati akizungumza,wasichana hawa walikuwa wameziba pua zao.
ITAENDELEA..............................................
Tags
simulizi