TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SHUJAA 02

ONYO: SIMULIZI INAHUZUNISHA SANA.

Story: SHUJAA
episode: 02
ILIPOISHIA....... 

Janeth alikuwa hana muda na wasichana wenzake. Marafiki zake kwa sasa ni wanaume pengine isingekuwa kuishi pamoja na Ester hata urafiki wao ungekuwa ushakufa maana tayari ulianza kudidimia.

ENDELEA NAYO..... 

Jumamosi hiyo ilikuwa Jumamosi kubwa iliyobeba maana halisi ya wikiendi kwa binti Janeth. Alikutana na mtu wake ambaye aliahidiana naye kukutana siku hii baada ya kushindikana siku ya nyuma.

Walikutana na Japhet,, huyu kijana hakuwa mwanafunzi bali ni mtu wa mtaa, walifurahi kwa kadiri walivyoweza na kwa namna waliyotaka, kwa mziki, pombe na mengine mengi ndani ya Baa moja iliyopo maeneo ya Kihonda.

Majira ya usiku sana ndipo alirudi nyumbani akiwa amelewa mno. Ilikuwa kazi kwa Ester kuanza kushughulika na mlango kumfungulia mwenzake. 

Kabla Janeth hajaingia, harufu ya pombe iliingia ndani na kuzipapasa pua za Ester. 

Hakika Ester alichefuka na kushtuka kuona kumbe hata pombe anatumia huyu mwenzake. Ilikuwa ngumu kuamini moja kwa moja lakini ushahidi ulikuwa mbele yake.

"Ester dada,,! binti mlokole"Janeth aliongea kilevi levi wakati huo ameegemea mlango.

"Ingia basi utabomoa mlango" alisema Ester na kuziba pua akitamani asiingie tu. Hata kile kitendo cha kumwambia aingie ni basi tu kwakuwa hakuwa na namna.

"Acha uharibike mimi nitalipa, kwani hela kitu gani??" aliongea huku anafungua kibegi na kutoa noti nyingi za elfu kumi kumi. Ester alitokwa na macho utadhani mjusi kabanwa na mlango.

Hajakaa sawa macho yake yalitua juu ya simu kubwa ya iPhone aliyoitoa Janeth kutoka kwenye kibegi kile.

"Haya ndio maisha, wewe endelea kumpa Bwana sifa akupe vitu kama hivi" aliongea tena kilevi na kucheka kwa dharau. Alitoka pale na kwenda kujitupa kitandani. 

"Ester wewe mlokole usitamani mali za mwingggnnn" aliishia kumumunya maneno kwani usingizi ulimbeba ghafla kutokana na uchovu wa hali ya juu.

Muda wote huo macho ya Ester yalikuwa kwa Janeth aliyejilaza. Yalikuwa macho yaliyojazwa na mshangao mkubwa juu ya mwenzake kulewa, kuwa na hela zote zile pamoja na simu kubwa. Kavitoa wapi???
Alipojiuliza hivyo akakumbuka kuwa pale ni mjini kama alivyoambiwa. Alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa.
Aliwaza namna ya kulala asijue, alale na mlevi??? Alitandika kanga chini na kuuvuta usingizi kwa tabu.

Siku zilisonga mbele kwa kasi na sasa Ilikuwa jumapili fulani majira ya saa 4,, wakati Ester anajiandaa kwenda kumpa sifa Mungu wake yeye Janeth alikuwa anaweka mambo sawa kwenda kufurahia raha za dunia. Ester alianza kutoka na kwenda kanisani kisha baadaye naye Janeth alitoka.

Kutokana na ibada kuwa ndefu pia mazoezi ya kwaya Ester alichelewa kurudi nyumbani. Alirudi majira ya saa moja usiku. Alishituka sana baada ya kufika nyumbani na kukuta kufuli linaning'inia mlangoni.

"Mmh!! Bado hajarudi tu" alisema na kwenda kuangalia mahali wanapoweka funguo siku zote. Hazikuwepo.

Ulikuwa mtihani mzito kwake hakujua anafanyaje na kama anazo mwenzake hizo funguo, atazipataje wakati hajui yuko wapi. Funda la hasira lilimkaba kooni. Alitamani kulia. Akiwa katika hali hiyo alishtushwa na sauti ya mpangaji mmoja wa kiume.

"Chukua simu ongea na mwenzako"

Ester alipokea simu na kusikiliza upande wa pili.
"Ester samahani bwana nilijisahau nikatoka na funguo,, njoo hapa fensi kona kwenye baa inaitwa Tushikamane. Chukua bodaboda nauli nitalipa" alieleza Janeth.
                            ★
Ester alifika na kuchukua funguo zile huku hasira zikipungua sasa.

"Chukua na hizi hela,,, ni zako" alisema Janeth na kumpatia mwenzake.

"Zimetoka wapi???"

"Wewe chukua" Janeth aliongea kwa ukali kidogo,, ilibidi Ester apokee japo kwa kusita.

"Haya nenda nyumbani lakini usiogope sawa Ester,, usiogope" alisema maneno yaliyompa maswali Ester na wasiwasi mwingi.

Alipanda tena bodaboda na kurudi nyumbani. Ilichukua dakika tano tu kufika.
Bado akili yake haikuwa sawa kabisa iliwaza hizo hela ambazo ni shilingi elfu hamsini tathilimu. Zimetoka wapi?? Ni zake,,, kwa kazi gani??? Hakujua.

Alifungua mlango haraka ili akapike maana hata njaa ilikuwa inamuuma. Aliingia ndani na kufunga mlango kisha alibonyeza swichi, taa ilitoa mwanga ulioenea chumba kizima.

"Mamaaaaaaaaaaaaa!!!" Ester alipiga kelele.

"Wewe binti mzuri acha kuogopa bwana" ilikuwa sauti ya kidume kilichokuwa kimejilaza kitandani, kidume hiki kilikuwa katika vazi la bukta na tisheti nyepesi. Kwa haraka haraka ukimtazama hakuwa anavuka miaka 25,, alikuwa na mwili umejazia jazia.

Alitoka pale kitandani na kuanza kupiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Ester aliyebaki anatetemeka kwa woga. Kutoka akimbie alishindwa kwani alishaufunga mlango. 
Ester aliziba macho asimtazame maana alihisi kama lisimba linamsogelea.

Mkono wenye nguvu ulianza kutembea mwilini mwake na kabla hajakaa sawa alibebwa msobe msobe hadi kitandani.

"Jamani nakufaaaa" alitoa sauti ya kulalamika kwa uchungu lakini sauti hii iliishia mle mle chumbani kwani kile chumba kilikuwa hakiruhusu sauti yoyote kutoka nje endapo mlango umefungwa. Kumbuka Ester alipoingia alifunga mlango.

                         ★

"Janeth mbona unaniangusha aisee"

"Sio kama nakuangusha George ila kama unavyofahamu yule Ester ulokole mwingi sana hivyo inanipa ugumu kuanza kumshawishi" alisema Janeth

"Ah!! Lakini hela yangu ushakula muda mrefu,,, ni wiki hadi sasa simpati huyo binti" alilalamika George na kuonesha wazi kuwa alichukia.

"Nivumilie kidogo basi leo akirudi kanisani namwambia"

"Hapana! Hizo ndio ahadi zako kila siku sasa nimechoka. Kama vipi nipatie hela yangu" alisema kwa hasira George,, Janeth alishtuka na kujiweka sawa pale kitandani. 

Hela yenyewe ameshatumia angerudisha vipi?? Hata kama angekuwa nayo hivi kabisa akubali kurudisha??

"Basi George unaonaje unitumie mimi tu,, tumia tu mwili wangu" alisema Janeth na kwenda kufunga mlango.

"Hapana! Mimi namtaka yule binti tu"

Mambo yaligonga mwamba,, Janeth alikosa cha kusema sembuse cha kufanya.

"Nimepata wazo, kwasababu mimi natoka leo basi nikufungie humu ndani halafu yeye atakaporudi kutoka kanisani unamalizana naye" alisema Janeth. George alifikiria kidogo kisha akasema. 

"Ni wazo zuri lakini vipi akipiga kelele?"

"Hiki chumba hakina shida cha msingi mlango na dirisha vifungwe tu basi hakutakuwa na tatizo lolote lile" alisema kwa kujiamini Janeth.

"Una uhakika??"

"Yes! Sasa hapo ushindwe mwenyewe tu"

George alifungiwa ndani wakati huo Janeth anatoka kwenda fensikona katika baa moja iitwayo Tushikamane bar.

"Hata hizi funguo ngoja niondoke nazo" alijisemea na kuchukua bodaboda hadi Fensikona wakati huo huku ndani George alikaa akiwa na hamu zake nyingi tu.

Alishajipanga kwa tukio ndio maana hata suruali yake aina ya jinsi aliivua na kubaki na bukta. 
Muda uliendelea kuyoyoma bila mtu anayemsubiri kufika. Mlango ungekuwa wazi angekata tamaa na kuondoka. Aondoke??? Angetokea wapi?? 
Njaa nayo ilianza kumkejeli. Alichungulia ndani ya sufuria tatu zilizokuwepo hapo ndani,, hazikuwa na chochote. "Hyaaaaaammm!!!!!" Alipiga muayo.

Kila muda aliangalia saa yake ya mkononi na ubaya zaidi simu aliiacha nyumbani kwenye chaji. Angekuwa nayo hapo angempigia Janeth arudi kumfungulia ili aondoke akale.

Majira ya saa moja usiku ndipo anashituka kusikia mlango unafunguliwa na kumuona binti aliyemsubiri kwa muda mrefu. Alikuwa na hasira naye hivyo alimbeba msobe msobe hadi kitandani.

Baada ya kutimiza hitaji lake alivaa nguo zake huyo aliondoka huku akijisifu.

"Laki moja yangu imeenda kwa haki,, mtoto alikuwa mbichi kabisa,, mimi ndio mfunguzi" 
Alichomaanisha alikijua mwenyewe sisi wengine tuendelee kusoma simulizi.

Huku nyuma Ester alikuwa na hali mbaya mno, sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibiwa, nayo maumivu hayakuona huruma, yalimtafuna kisawa sawa hata kutembea hakuweza.

Alijaribu kuinuka ili akausafishe mwili wake kuondoa damu zilizotapakaa, hakuweza kupiga hata hatua moja, alichechemea kidogo na kuanguka chini.

Majira ya saa sita usiku Janeth alirudi.

Muda huo wa saa 6 Janeth aliporudi bado Ester hali yake haikuwa nzuri, alijikalia chini kama kiwete asiye na uwezo wa kuinuka. Uso ulijawa na machozi. Hakutaka hata kumtazama mwenzake, alimuona kama jambazi sugu mwenye roho ya kikatili ambaye anaweza kukuua kwa sekunde chache.

Ester alitazama upande mwingine huku akijitahidi kuzishinda hasira kali zilizokuwa zinapanda kwa kasi dhidi ya Janeth aliyekuwa ameingia huku anayumba maana alilewa.

"Wewe binti mlokole,, binti wa bwana unalia nini" aliongea Janeth,, namna alivyoongea alidhihirisha amelewa haswaa. Ester alizidi kupata hasira zilizokuwa zinampa nguvu ya kunyanyuka pale na kumrarua rarua. Uwezo wake kuzishinda ulikuwa mkubwa kuliko nguvu ya hasira.

"Halafu umeanza uchafu,, unachafua ndani hata usafi hufanyi wala huogi binti mlokole mchafu" alisema tena huku akiyumba , alimpiga kofi mwenzake kisha yeye aliangukia kitandani na kupitiwa na usingizi mzito uliochangiwa na uchovu mwingi.

Ester alilia. Alilia sana kila alipokumbuka yote aliyofanyiwa siku hiyo.
"Nimekukosea nini Mungu??? Mbona hukutaka kuniepusha na huu ubaya,, kwanini umeruhusu hili litokee.? Naumia mimi" Alilia mno kila alipokumbuka kuwa usichana wake haupo tena.

Usichana kwa msichana ni kama dhahabu ama mali yoyote yenye thamani kubwa sana na ndio maana wengi huumia sana wanapopoteza usichana wao hata kama waliupoteza kwa ridhaa na matakwa yao wenyewe, hulia na kujilaumu sembuse kuupoteza usichana kwa njia ya ukatili??

Ester alilia kila alipokumbuka kuwa usichana wake umepotea tena umepotezwa na mtu asiyemfahamu zaidi ya kuambulia kuiona sura ambayo yenyewe inaweza kupotea katika kumbukumbu.

Katika kipindi chote cha maisha yake hadi hapo yupo kidato cha sita hakuwahi kukutana na mwanaume yeyote,, alijichunga sana kufuatia kauli ya kila mara kutoka kwa Mama yake iliyokuwa inamsisitiza kujitunza na kuutunza usichana wake kwa ajili ya mume wake wakati atakapoolewa. Leo usichana wake haupo.

"Jitunze binti yangu,,, tunza usichana wako maana hata wanaume wanapenda wanawake waliojitunza" hii ilikuwa kauli ya Mama yake.

"Nani atanioa sasa?? Nitamwambia nini Mama?? Kwani nimekosea nini mimi jamani aah!!??" Ester alilia kama mtoto mdogo. Aliona dunia imekuwa mzigo mzito, tena uzito huu umeegamia kwake na kumng'ong'a.

Usiku huu hakulala wala hakufanya chochote hata kwenda kujisafisha alishindwa. Angetembeaje?? 
Mawazo yalikuwa mengi mno, yalimtesa kichwa na kumzawadia kilio kisichoisha, kilio kilichofanya akose usingizi. Alilia huku anahisi kuna kitu kinamkaba shingoni, alitambua ni hasira.

Saa nayo bila huruma iliendelea kusonga mbele japo ilijua tu kuwa kuna mtu hajalala, ilikuwa saa nane na bado sekunde ziliendelea kukimbizana kwa madaha. Wakati huo hata chembe ndogo sana ya usingizi haikuwepo machoni wala kichwani mwa Ester. Janeth alikuwa anakoroma,, miguu kaitupa huko na huko.

Baada ya kuwaza sana ndipo akakumbuka kuhusu zile hela elfu hamsini alizopewa na Janeth alipofuata funguo.

"Nimeuzwa mimi" aliendelea kulia.

Majira ya saa kumi na moja, usingizi ulimuonea huruma,, alijilaza pale chini bila kujua.
                            ★
Ni Jumatatu sasa, pengine ni kutokana na kuchelewa kulala ndio maana aliamka majira ya saa tatu asubuhi.

"Mungu wangu nimechelewa shule" alitazama huku na huku, hakumuona mwenzake, alikuwa peke yake.

Alisimama haraka ili ajiandae,,, Loooh!!! Ester alisahau yote. Maumivu aliyoyapata baada ya kuinuka haraka yalimkumbusha kilichotokea jana usiku. Isingekuwa kushikilia kitanda basi angeanguka vibaya sana. Bado hali ilikuwa mbaya.

Hii siku ilipita Ester analia tu, hakwenda shule hata mwenzake aliporudi hakutaka kuongea naye. Angeongea naye nini???
Hata kula hakula, kilio na machozi vilikuwa chakula chake. 

Jumanne nayo ilipita hata Jumatano pia ilipita,, mwili ulikosa nguvu kwa kutokula, macho yalivimba na yalikuwa mekundu kwa kulia. Ila ilikuwa afadhali ndani ya mwili wake, Maumivu yalipungua kabisa.
Alhamisi alijiandalia uji na baada ya kunywa alijitajidi kufika shule. 

Huku sasa ilikuwa shida,, licha ya kumwambia mwalimu kuwa alikuwa anaumwa lakini hakusikilizwa.

"Leta kibali cha daktari,," alisema mwalimu David ambaye alikuwa zamu.

Ester alikosa cha kusema maana hata hicho kibali hakuwa nacho. Alitamani aseme ukweli wa mambo lakini aliogopa na kuona aibu.

"Nyie ndio wahuni hamtaki kuja shule mnaenda kudanga. Na tunawasaka sana watu kama nyinyi mnaoharibu sifa ya shule yetu, sasa leo utanitambua" alifoka mwalimu David na kumvuta mkono Ester hadi ofisini.

Bakora kali zilianza kusikika zikirindima ndani ya ofisi.

USIKOSE KUFUATILIA MKASA HUU....

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post